Elizabeth alianza safari yake ya ujasiriamali akiwa na mtaji mdogo sana – laki mbili tu (200,000/=). Kwa macho ya wengi, hii ingekuwa ndoto ngumu kufanikisha. Lakini Elizabeth aliamua kuthubutu, kuamini kwenye ndoto zake na kuanza kidogo alichokuwa nacho.
Safari yake haikuwa rahisi. Kama vijana wengi wa Kitanzania, changamoto zilikuwa nyingi – mtaji mdogo, elimu ya biashara haitoshi, na kukata tamaa kulimkaribia. Lakini TADB – Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania – waliona juhudi na ndoto yake. Wakamshika mkono.
Kwa msaada wa TADB, Elizabeth alipata mtaji wa kuendeleza shughuli zake. Alipewa elimu ya namna ya kusimamia biashara yake vizuri, kuikuza, na kuifanya iwe endelevu. Leo hii, Elizabeth si yule tena wa kuanza na laki mbili. Amefanikiwa kupiga hatua kubwa kibiashara na sasa ni mfano wa kuigwa na vijana wengine wengi. Anaelimisha na kuhamasisha wajasiriamali wenzake – kwamba inawezekana.
Ujumbe muhimu kwa vijana wa Kitanzania: “Ukiona fursa – changamkia! Ukipewa msaada – usiutazame kama msaada wa kawaida, bali kama chachu ya mafanikio. Thubutu, jifunze, na usikate tamaa.” Elizabeth ni ushahidi hai kuwa TADB sio tu benki – bali ni mshirika wa ndoto za Watanzania.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+