DKT. NDUMBARO AKITATUA MIGOGORO KATIKA BANDA LA KATIBA NA SHERIA: SABASABA 2025

Katika maonyesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba, Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, ametembelea banda la Wizara yake na kushuhudia kwa vitendo utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi.

Dkt. Ndumbaro ametumia fursa hiyo kusikiliza hoja za wananchi waliowasilisha malalamiko mbalimbali, yakiwemo ya migogoro ya ardhi, mirathi, ndoa, pamoja na haki za watoto, na kutoa miongozo ya moja kwa moja kwa vyombo husika.

Tazama video hii ujionee namna Serikali inavyosogeza huduma kwa wananchi, kusikiliza matatizo yao na kutafuta suluhisho kwa wakati.

📍 Mahali: Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Sabasaba – Dar es Salaam

📆 Maonesho ya Sabasaba 2025

📌 “Huduma za Kisheria kwa Wote, Bila Ubaguzi”

👉 Subscribe, Like na Share kwa taarifa zaidi kuhusu haki, sheria na huduma za kisheria zinazotolewa na Wizara ya Katiba na Sheria.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *