MALEZI BORA NI SULUHISHO LA KUDUMU DHIDI YA URAIBU KWA WATOTO – MOHAMED JUMAhttps://youtu.be/1xzUwyOshro

Mohamed Juma, Meneja wa nyumba ya Mamas and Papas House iliyopo Mkuranga, Dar es Salaam, amesema kuwa moja ya chanzo kikuu cha uraibu katika jamii ni ukosefu wa malezi bora kwa watoto kuanzia wakiwa wadogo. Nyumba hiyo imejikita katika kutoa elimu kuhusu malezi na afya ya akili kwa watu walioathirika na uraibu, huku ikitoa ushauri kwa wazazi na walezi kuhusu namna ya kuzuia tatizo hilo.

Akieleza tofauti kati ya malezi na matunzo, Mohamed alisema: “Matunzo ni kuhakikisha mtoto anapata mahitaji ya msingi kama chakula, malazi, mavazi na elimu. Lakini malezi ni zaidi ya hayo yanahusu maadili, tabia, nidhamu na namna mtoto anavyojiandaa kutekeleza majukumu ya kifamilia na ya binafsi katika maisha.”

Amesisitiza kuwa wazazi wanapaswa kufahamu kuwa watoto hujifunza kwa kuangalia. Kwa hiyo, ni muhimu kuacha kufanya vitendo ambavyo watoto wanaweza kuiga kama vile kutumia lugha chafu, kutokuheshimu muda au kuwa na mienendo isiyofaa.

Mohamed ameongeza kuwa ni muhimu wazazi kujali mambo kama muda wa kulala wa mtoto, muda wa kurudi nyumbani, muda wa kucheza na pia kuepuka kupeleka watoto maeneo ya starehe yasiyo na maadili, kwani hilo huongeza uwezekano wa watoto kuingia katika vishawishi vya uraibu mapema.

Ametoa wito kwa wazazi kuwa mstari wa mbele katika kujenga kizazi chenye afya ya akili bora kwa kuwekeza kwenye malezi yenye kufuata maadili, uwajibikaji na upendo wa kweli.

Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”

#DCEA

#OktobaTunatiki

#Sabasaba2025

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *