Maktaba ya Kila Siku: July 3, 2025

ASASI ZA KIRAIA ZAIPONGEZA DCEA KWA USHIRIKIANO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Viongozi wa asasi mbalimbali za kiraia zinazotoa elimu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya wameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana nao bega kwa bega katika mapambano dhidi ya janga hilo linaloathiri maisha ya vijana wengi nchini. Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki ni …

Soma zaidi »

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi

Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa wananchi kwa ujumla na ni moja ya sababu inyowezesha maendeleo ya Taifa kwenda kwa kasi. Amesema hayo leo Alhamisi (Julai 03, 2025) wakati wa uzinduzi wa Benki ya Maendeleo PLC, kuwa Benki kamili ya kibiashara, …

Soma zaidi »

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini kwa kuwa anawaongoza wananchi wenye dini ambao dini zao wanaziheshimu na hivyo asingependa kuona haki zao zinanyimwa kwa namna yoyote ile

Dkt. Biteko amesema hayo Julai 3, 2025 jijini Dodoma wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). “Mheshimiwa Rais Samia anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini na ninyi ni mashahidi amekuwa akiwaalika ili tuzungumze masuala mbalimbali ya kitaifa …

Soma zaidi »