VIJANA WAIPONGEZA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KWA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Anna Mathayo Phanga kutoka taasisi ya Blue Cross Society of Tanzania ya jijini Arusha amesema serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa ya kuokoa maisha ya Watanzania kwa kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika kinga na tiba dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya. Ameeleza kuwa hatua hizi zimeleta matumaini mapya kwa jamii na kusaidia kuwaokoa vijana waliokuwa katika hatari ya kupotea.

Aidha, Anna ameipongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele kuhimiza jamii yenye afya na maisha bora bila dawa za kulevya. Amesema uongozi wake umekuwa wa kishujaa na wa kuigwa katika mapambano haya.

Kwa upande wake, Shaaban Juma Rashid, ambaye aliwahi kuwa mtumiaji wa dawa za kulevya kwa zaidi ya miaka minane, amesema anamshukuru Mungu kwa kumuwezesha kupona baada ya kupatiwa huduma katika kituo cha Utulivu Sober House.

Shaaban amempongeza Rais Samia kwa kuendelea kuwekeza katika Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), hatua iliyomuwezesha kupata msaada na kurejea katika maisha ya kawaida.

Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”

#DCEA #OktobaTunatiki

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *