ASASI ZA KIRAIA ZAIPONGEZA DCEA KWA USHIRIKIANO KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA

Viongozi wa asasi mbalimbali za kiraia zinazotoa elimu ya athari za matumizi ya dawa za kulevya wameipongeza Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa kushirikiana nao bega kwa bega katika mapambano dhidi ya janga hilo linaloathiri maisha ya vijana wengi nchini.

Miongoni mwa taasisi zilizoshiriki ni ANT Alcoholism and Drug Addiction Organization, Nugget Development in Tanzania (NDT), T.O.G.T, T.D.P.N, Youth Achievement of Tanzania, pamoja na Action Plan Organization.

Viongozi wa taasisi hizo wamesema mafanikio ya jitihada zao katika kutoa elimu, kusaidia waathirika na kuhamasisha jamii yasingefikiwa bila ushirikiano wa karibu na DCEA, ambao umeendelea kuwajengea uwezo, kuwapa fursa ya kushiriki kampeni mbalimbali na kusaidia kufikisha elimu kwa jamii ya Watanzania hasa vijana.

Wamesema kuwa kwa mara ya kwanza, jamii imeanza kuelewa kuwa dawa za kulevya si tu tatizo la mtu binafsi, bali ni changamoto ya kijamii inayohitaji ushirikiano wa pande zote serikali, familia na taasisi za kijamii.

Wamezitaka taasisi nyingine kuunga mkono jitihada hizo huku wakiahidi kuendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano haya, wakisisitiza kuwa “kila kijana aliyeokolewa ni taifa lililookolewa.”

Kauli mbiu: “Wekeza kwenye Kinga na Tiba dhidi ya dawa za kulevya”

#DCEA #OktobaTunatiki

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *