Maktaba ya Kila Siku: December 2, 2025

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe. William Lukuvi, amewahakikishia Watanzania kuwa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARVs) zinapatikana kwa asilimia 100 nchini na zinatolewa bila malipo kwa watu wote wanaoishi na VVU (WAVIU).

Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa Tamko la Serikali kuhusu Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kwa mwaka 2025 yamefanyika chini ya kaulimbiu: “Imarisha Mwitikio, Tokomeza UKIMWI”. Waziri Lukuvi amesema upatikanaji wa dawa hizo umeendelea kuimarika, huku idadi ya WAVIU wanaotumia Dawa za ARV ikiongezeka kutoka …

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kabla ya kuzungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.

Soma zaidi »

RAIS DKT. SAMIA AKIZINDUA TUME HURU YA UCHUNGUZI WA MATUKIO YA UCHAGUZI MKUU, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Tume Huru ya Kufanya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjiifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025, Ikulu Chamwino, Dodoma, tarehe 20 Novemba, 2025. 📌 Usikose kufuatilia hotuba na matukio yote muhimu hapa …

Soma zaidi »