Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameongoza hafla ya kihistoria ya uzinduzi wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 jijini Dodoma.
Kupitia hotuba yake ya kina na yenye mwelekeo, Mhe. Rais ameeleza dhamira ya Serikali kuhakikisha Tanzania inafikia maendeleo jumuishi, yenye ushindani wa kiuchumi, ustawi wa jamii, na ulinzi wa mazingira ifikapo mwaka 2050. Amehimiza ushirikiano baina ya sekta ya umma, binafsi, vijana, wanawake, na wadau wa maendeleo ili kufanikisha maono haya.
Dira hii ni mwongozo wa kitaifa utakaosaidia kupanga sera, mipango, na bajeti katika ngazi zote za utawala kwa kipindi cha miongo mitatu ijayo, ikilenga kujenga Taifa lenye uchumi imara, watu wenye maarifa na ustawi wa maisha kwa wote.