“Tangu kuanza kwa mradi wa EACOP mwaka 2022 hadi sasa, jumla ya Watanzania 9,194 wamepata nafasi za kufanya kazi ndani ya mradi na hivyo kuwa fursa kwao ya kujipatia kipato, mwaka 2024 kampuni ilitoa mafunzo maalumu kwa Vijana 170 na kuwapatia kazi kwenye mradi, Vijana wengine 110 wapo katika masomo …
Soma zaidi »Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025. Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri ni cha mwisho cha Serikali ya Awamu ya Sita kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka kwenye picha ya pamoja na Mawaziri mara baada ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri cha Serikali ya Awamu ya Sita kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania ina umeme wa kutosha hatua ambayo imechangiwa na kukamilika kwa Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme ukiwemo Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ambao pekee unazalisha Megawati 2115
Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo Julai 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya kuzalisha umeme kwa gesi asilia katika vituo vya Kinyerezi I, Kinyerezi I Extension na Kinyerezi II ambapo amesema licha ya kazi kubwa inayofanywa na TANESCO yapo baadhi ya maeneo yalikua na changamoto …
Soma zaidi »Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini kwa kuwa anawaongoza wananchi wenye dini ambao dini zao wanaziheshimu na hivyo asingependa kuona haki zao zinanyimwa kwa namna yoyote ile
Dkt. Biteko amesema hayo Julai 3, 2025 jijini Dodoma wakati akimwakilisha Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano Mkuu wa 32 wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT). “Mheshimiwa Rais Samia anapenda kufanya kazi na viongozi wa dini na ninyi ni mashahidi amekuwa akiwaalika ili tuzungumze masuala mbalimbali ya kitaifa …
Soma zaidi »🅻🅸🆅🅴 :🔴MHE. RAIS DKT. SAMIA AKISHIRIKI MKUTANO MKUU CCM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Akishiriki Mkutano Mkuu CCM Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center Dodoma, leo tarehe 29 Mei, 2025. #ijuesheria #ijuesheria #section4wakilitv #bunge #ijuesheria #section4wakilitv #bunge #bungenidodoma #chadema #chademamedia #tls #tundulissu #tls #mwabukusi #uchaguzimkuu2025 #uchaguzi #uchaguzimkuu
Soma zaidi »DKT. BITEKO AWATAKA WAZAZI KUTUNZA FAMILIA ZAO.
“ Mtoto ni zao la matokeo ya wazazi wawili, Naomba wazazi tuthamini kuwa mtoto ni mtu muhimu na anahitaji kulelewa, tukumbuke kuwa tumefika hapa kwa kuwa wako wazazi walivumiliana na wakatulea katika familia na sisi tusiwe watu wa kutelekeza familia zetu, ni wajibu wa kila mmoja kujua kuwa familia ni …
Soma zaidi »