🔴 LIVE: SHEREHE YA 73 YA KUWAKUBALI NA KUWAPOKEA MAWAKILI WAPYA
HUYO MTU ANAITWAJE …. ?
#SisiniTanzania #nchiyangukwanza #TanzaniaNiwajibuwetu #Nchiyetufahariyetu #tanzania #SSH #kazinaututunasongambele #matokeochanya #katibanasheria #mslac @samia_suluhu_hassan @mawasilianoikulu8747
Soma zaidi »NEMC yasaini makubaliano ya awali na Kampuni ya United Platform Solution (UPS) kwa ajili ya kuanzisha mfumo wa kidigitali wa ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira katika miradi yote ya maendeleo nchini. Makubaliano hayo yamefanyika Disemba 04, 2025 katika ukumbi wa mikutano NEMC.
SISI WATANZANIA TUNAWEZA …
NEMC leo imeungana na Jumuiya ya kimataifa kuadhimisha Siku ya Walemavu Duniani kwa kutoa wito wa kuimarishwa kwa mazingira jumuishi na rafiki kwa watu wote, hususani watu wenye ulemavu.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi.
Soma zaidi »Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa silaha za jadi Mkuki kutoka kwa Mzee Ndijina Ndilanza Ndilito, mwakilishi wa wazee wa Tanzania Bara pamoja na ngao kutoka kwa Bi. Ubwa Hamis Ally mwakilishi wa Wazee wa Zanzibar kama ishara ya kulinda na kuitetea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Mhe. Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.
Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira. Aidha, Lord …
Soma zaidi »Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Mhe. William Lukuvi, amewahakikishia Watanzania kuwa dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARVs) zinapatikana kwa asilimia 100 nchini na zinatolewa bila malipo kwa watu wote wanaoishi na VVU (WAVIU).
Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akitoa Tamko la Serikali kuhusu Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kwa mwaka 2025 yamefanyika chini ya kaulimbiu: “Imarisha Mwitikio, Tokomeza UKIMWI”. Waziri Lukuvi amesema upatikanaji wa dawa hizo umeendelea kuimarika, huku idadi ya WAVIU wanaotumia Dawa za ARV ikiongezeka kutoka …
Soma zaidi »
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+