RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN AFUNGUA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA MJINI MAGHARIBI-ZANZIBAR 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Daktari. Samia Suluhu Hassan, amefungua rasmi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini Magharibi iliyopo Lumumba Kisiwani Zanzibar.
 
Rais Dkt. Samia amefungua hospitali hiyo leo tarehe 10 Januari, 2024 ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake Kisiwani humo katika kuelekea Maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar siku ya tarehe 12 Januari, 2024.
 

Hospitali hiyo yenye ukubwa wa ghorofa 5 itakuwa sehemu kubwa ya kusaidia utoaji wa huduma ya Afya kwa asilimia 100% kutokana na uwepo wa vifaa mbalimbali vya matibabu vya kisasa.

Mara baada ya kufungua Hospitali hiyo, Rais Dkt. Samia amezungumza na Viongozi, Wageni waalikwa na Wananchi kwa ujumla na kuhimiza kutunzwa kwa Vifaa tiba hivyo pamoja na utunzaji wa Mazingira.

 #NA HAYA NDIYO MATOKEO CHANYA+

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *