Wafanyabiashara ndogo ndogo (Machinga) mkoani Morogoro wameonyesha mshikamano wao na Rais Samia Suluhu Hassan katika juhudi za kujenga taifa. Wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono miradi ya maendeleo na sera za serikali, wakikemea vikali wale wanaopinga juhudi za kuleta maendeleo nchini. Machinga hao wamesisitiza kuwa wako tayari kushirikiana na serikali katika kuhakikisha nchi inasonga mbele na kukuza uchumi, huku wakieleza kuwa vitendo vya wapinga maendeleo havina nafasi katika Tanzania ya leo. Mkutano huu umeonyesha nia thabiti ya wananchi katika kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kujenga uchumi imara na maendeleo endelevu.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+