SINGIDA MASHARIKI KUPATA MAJI YA UHAKIKA

Jumla ya visima 13 vya maji vimejengwa katika Jimbo la Singida Mashariki ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) iliyoahidi kumtua mama ndoo ya Maji kichwani.

Akizungumza mara baada ya kukagua kazi ya uchimbaji wa kisima kirefu cha maji katika kijiji cha Munkinya, mbunge wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amemshukuru Rais Dkt John Magufuli kwa kuendelea kutekeleza ahadi aliyoitoa.

“Mwaka jana nilipoingia bungeni kwa mara ya kwanza swali langu la kwanza lilihusiana na kero ya maji katika jimbo letu,nashukuru aliyekuwa naibu waziri wa maji Jumaa Aweso aliahidi kuja kuangalia hali ilivyo na alitekeleza ahadi yake,

“Rais Dkt Magufuli aliposikia kero hii alitoa maelekezo ya kutolewa kwa fedha na kazi ikaanza mara moja na sasa hali imebadilika kwa kipindi kifupi na wananchi wanatarajia kupata maji,”alisema.

Amesema kazi hiyo ilianza Mwaka jana baada ya serikali kuidhinisha kiasi cha Sh Bilioni 3.7.

“Huu ni muendelezo wa kazi iliyoanza mwaka jana baada ya serikali kutupa mgao wa visima 15 kwenye jimbo letu la Singida mashariki,na mpaka sasa tayari vijiji 13 vimeshachimbwa visima virefu na miundombinu inaendelea kujengwa ili wananchi waanze kutumia maji safi na salama,”alisema.

Ametaja vijiji vilivyochimbiwa visima virefu mpaka sasa kuwa ni Mang’onyi,Matare,Mbwanjiki,Kipumbuiko,Munkinya,Minyinga,Unyanghumpi,Kinku,Lighwa,Mampando,Sakaa na Mkunguakihendo.

Amewaomba wananchi kutunza miradi hiyo inayojengwa kwa ajili yao ili iweze kudumu kwa muda mrefu na iwe na faida kwao na kwa vizazi vijavyo.

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi

Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *