Waheshimiwa Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali wakifuatilia uwasilishwaji wa maelezo ya Mradi kutoka kwa Meneja Mradi wa Julius Nyerere Mhandisi Stephen MandaMradi wa Kufua Umeme wa Julius Nyerere ni muhimu kwa maendeleo ya Afrika, Tanzania tunaingia katika Historia ya Dunia kwa kuwa na Bwawa kubwa kati ya mabwawa makubwa 70 Duniani – Balozi Abdallah Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani.Mradi wa Kufua Umeme kwa maji wa Julius Nyerere utaondoa tatizo la umeme ambalo limekuwa likitukabili muda mrefu, pia kuna fursa za uwekezaji kwenye maeneo ya mradi ambazo zitatufikisha uchumi wa Viwanda – Balozi Dkt. Wilbroad Slaa, Balozi wa Tanzania nchini Sweden.