WAZIRI MKUU AFUNGUA JENGO LA TAASISI YA KARUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA
Matokeo ChanyA+
January 9, 2019
Tanzania MpyA+, Waziri Mkuu
1,524 Imeonekana
- Asema kukamilika kwa taasisi hiyo kutakuwa na manufaa makubwa kwa jamii
- Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua Jengo la Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia (KIST), wilaya ya Magharibi ‘B’ lililojengwa kwa ghararama ya sh. bilioni 4.2.
- Waziri Mkuu amesema kulingana na maendeleo ya kiteknolojia na mahitaji ya soko uongozi wa KIST ujipange kutoa mafunzi ya biomedical Engineering na kuimarisha mafunzo ya matengenezo ya ndege na urubani katika ngazi ya stashahada.
- Awali, Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Amali, Riziki Pembe Juma alisema Wizara yake itaendeleza taasisi hiyo ili kuwaendeleza vijana na baadae waweze kujiajiri na kuajiri.Alisema vijana wanaohitimu mafunzo ya fani mbalimbali katika taasisi hiyo wanapewa mikopo ya masharti nafuu na Serikali baada ya kujiunga kwenye vikundi.
- Waziri Huyo, alisema wahitimu hao kabla ya kupewa mikopo wanaandika andiko la miradi ambayo watakwenda kuitekeleza ambapo tayari vikundi zaidi ya 10 vya vijana vimeshawezeshwa.