Gari iliyotoelwa na Mbunge wa Dodoma Mjini,Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge akiungumza wakati wa utoaji gari hilo.
Mbunge wa jimbo la Dodoma mjini Mh Anthony Mavunde ametekeleza ahadi yake ya kuwapatia wananchi wa jimbo hilo gari la kuhudumia shughuli za mazishi ambalo litatumiwa na wananchi wote bila gharama yoyote.
Gari hilo maalum la huduma za mazishi limekabidhiwa leo kwa wananchi wa Dodoma chini ya uratibu wa Ofisi ya mbunge na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Dodoma Mjini ambapo Mbunge Mavunde amewashukuru wamiliki wa vituo vya G.88 NJOMBE FILLING STATION (NFS) na GAPCO kwa kujitolea mafuta lita 150 kwa mwezi kama sehemu ya mchango wa uendeshaji wa gari hilo.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr.Benilith Mahenge ambaye amempongeza Mbunge Mavunde kwa jitihada kubwa ya kuwahudumia wananchi na kutaka wanachi hao kulithamini na kutoa ushirikiano kwa Mbunge huyo.
Mbunge wa Dodoma Mjini,Anthony Mavunde ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu,wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bilinith Mahenge
Akishukuru kwa niaba ya Wazee wa Dodoma,Katibu wa Baraza hilo Mzee Makuberi amempongeza Mbunge Mavunde na kushangazwa na kasi ya maendeleo ndani ya muda mfupi katika Jimbo la Dodoma Mjini.