Matokeo ChanyA+

Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+.

UINGEREZA YAAHIDI KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA TANZANIA

Uingereza imeihakikishia Tanzania kuwa itaendelea kuwa mshirika wake katika masuala mbalimbali ya ubia wa maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha wawekezaji wengi kutoka Uingereza kuwekeza Tanzania kama moja ya hatua za kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Tano ili iweze kufikia azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati …

Soma zaidi »

WAKANDARASI TUMIENI VIJANA WANAOMALIZA JKT, KUJENGA MIRADI YA UMEME

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu amewashauri wakandarasi nchini kuwatumia vijana wanaomaliza mafunzo katika jeshi la kujenga taifa wenye  taaluma na ujuzi mbalimbali ikiwemo sekta ya Nishati ya Umeme. Mgalu alisema idadi kubwa ya vijana wanaohitimu mafunzo ya JKT wanakuwa na nidhamu, pamoja na uzalendo  katika kutekeleza majukumu yao  kwa …

Soma zaidi »

RAIS MUSEVENI KUFANYA ZIARA YA SIKU MOJA NCHINI

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kesho Jumamosi tarehe 13 Julai, 2019 atafanya Ziara Binafsi ya siku 1 moja hapa nchini. Mhe. Rais Museveni atamtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kijijini kwake Mlimani katika Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Akiwa …

Soma zaidi »

JAFO AONGEZA SIKU 30 UKAMILISHAJI WA HOSPITAL ZA WILAYA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ametoa siku 30 kwa Halmashauri zote zinazoendelea na ujenzi wa Hospitali za Wilaya kukamilisha kazi zote za Ujenzi ifikapo Julai 30,2019. Jafo ameyasema hayo wakati alipotembelea Hospital ya Wilaya ya Singida inayojengwa katika eneo la …

Soma zaidi »

PROF.KABUDI ASHIRIKI MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

Tanzania imeshiriki mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola ambao umelenga kujadili utekelezaji wa maazimio na vipaumbele vya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo ikiwemo masuala ya utawala bora,usalama,biashara pamoja na namna kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na utunzaji wa mazingira. Akichangia katika majadiliano juu ya …

Soma zaidi »

MKANDARASI ANAYESAMBAZA UMEME KIBONDO ATAKIWA KUONGEZA KASI

Naibu Waziri wa Nishati,Subira Mgalu,amesema haridhishwi na kasi ya usambazaji wa umeme vijijini inayofanywa na  mkandarasi wa Kampuni ya  Urban and Rural Engineering Services, wilayani Kibondo mkoani Kigoma. Mgalu ametoa kauli hiyo,kwenye mkutano na wananchi  wakati  alipofanya  ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji wa umeme vijijini wilayani humo  na kuwasha …

Soma zaidi »

SERIKALI YATOA MILIONI 700 KUSAIDIA KAZI WABUNIFU NCHINI

Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema Serikali kupitia Tume ya Tafa ya Sayansi na Teknolojia ( COSTECH) imetoa kiasi cha Tsh Milioni 700 kwa wabunifu 60 ili kuendeleza tafiti na bunifu zao na kuleta tija na manufaa kwa Taifa. Akizungumza leo Jumatano (Julai 10, 2019) …

Soma zaidi »

SHILINGI BILIONI 600 KUONDOA TATIZO LA UPATIKANAJI MAJI SAFI NA SALAMA TABORA

Manispaa ya Tabora itaanza kupata maji safi na salama wakati wote baada ya kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji toka Ziwa Victoria utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 600. Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mkoa wa Tabora (TUWASA), Mhandisi Mkama Bwire ameeleza hayo kwa Maafisa …

Soma zaidi »