Maktaba ya Kila Siku: December 3, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa silaha za jadi Mkuki kutoka kwa Mzee Ndijina Ndilanza Ndilito, mwakilishi wa wazee wa Tanzania Bara pamoja na ngao kutoka kwa Bi. Ubwa Hamis Ally mwakilishi wa Wazee wa Zanzibar kama ishara ya kulinda na kuitetea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.

Soma zaidi »

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC) Mhe. Lord Hugo Swire, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Desemba, 2025.

Rais Dkt. Samia pamoja na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Lord Hugo Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira. Aidha, Lord …

Soma zaidi »