KAZI INAENDELEA YA KUSIMIKA MABOMBA YA KUTOLEA MAJI KATIKA MRADI WA UMEME WA JNHPP



Kazi ya usimikaji wa bomba (Draft tube) sehemu ya chini kabisa kwenye mashine nambari 9 imeanza Agosti 17, 2021, katika mradi wa kufua umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), bomba hizo zitatumika kutolea maji katika mitambo ya kufua umeme na kuyarudisha mto Rufiji kwa ajili ya matumizi mengine.

Hii ni hatua kubwa iliyofikiwa baada ya kukamilika kwa uundwaji wa bomba hizi zinazofungwa katika kitako cha msingi wa zege, kilichopo eneo la mita 42.7 juu ya usawa wa bahari.

Usimikaji wa bomba hizi ndio utawezesha kuanza kwa ufungaji wa sehemu za juu za mashine (turbine) na kisha jenereta za kufua umeme.

Unaweza kuangalia pia

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Tanzania ina umeme wa kutosha hatua ambayo imechangiwa na kukamilika kwa Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme ukiwemo Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) ambao pekee unazalisha Megawati 2115

Naibu Waziri Mkuu ameyasema hayo Julai 10, 2025 wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *