RC KUNENGE APOKEA MAGARI 20 NA KONTENA 65 ZA KUHIFADHI TAKA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge March 03 amepokea Magari 20 na Kontena 65 za kuhifadhi taka zenye thamani ya Shilingi bilioni 4.1 ambapo amewahimiza wakazi wa Dar es salaam kuhakikisha wanazingatia suala la usafi wa mazingira.

Akipokea Magari hayo kwenye Bandari ya Dar es salaam, RC Kunenge ameyagawa kwa Halmashauri zote za Dar es salaam ambapo Halmashauri ya Jiji imepatiwa Magari 5, Manispaa ya Temeke Magari 8, Kinondoni Magari 5, Ubungo Gari 1 na Kigamboni Gari 1.

RC Kunenge amewaelekeza Wakurugenzi wa Manispaa zote kuhakikisha suala la usafi linapewa kipaombele huku akitaka magari hayo kutunzwa ili yadumu Muda mrefu na kutatua kero ya usafi.

Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi kuepuka tabia ya kutupa taka kwenye mitaro na mito kwani kwa kufanya hivyo wanasababisha mitaro kuziba huku akisema watakaohusika kuchafua mazingira Sheria itafuata mkondo.

Kwa upande wake Mratibu wa Miradi ya Bank ya Dunia chini ya TARURA na DMDP Humphrey Kanyenye amesema lengo la miradi wanayosimamia ni kuhakikisha wanaboresha mazingira ya Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira kuwa Safi.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *