UJENZI WA STESHENI YA MOROGORO YA RELI YA KISASA (SGR) UMEFIKIA ZAIDI YA ASILIMIA 70

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Jumapili Novemba 29, 2020, amewaongoza Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kukagua ujenzi wa stesheni ya Morogoro ya Reli ya Kisasa (SGR).

Katika ziara hiyo, Dkt. Abbasi alieleza kuridhishwa na kasi ya kukamilisha stesheni hiyo ambayo imefikia zaidi ya asilimia 70 huku ujenzi wa jumla wa SGR kwa kipande cha Dar-Moro ukiwa zaidi ya asilimia 90.

“Huu ulikuwa miongoni mwa miradi ambayo wananchi walimwamini Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa ndiye kiongozi pekee na wa aina yake anayefaa na mwenye maono thabiti ya kuja kuukamilisha katika Miaka Mitano Tena.

“Sisi tumekuja kujiridhisha kazi zinavyoendelea na hakika tumeona kweli leo ni Jumapili na saa hizi inakwenda jioni lakini watu wako kazini wanawajibika basi na kazi iendelee,” alisema Dkt. Abbasi.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *