Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja ametembelea mradi wa kupeleka Majisafi na salama katika mji wa Chalinze wenye thamani ya Bilioni 16 unaotarajiwa kumalizika mwezi Aprili 2020.Amewahakikishia wakazi wa Chalinze tatizo la maji katika mji wao kuwa historiaMtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), Cyprian Luhemeja wa pili toka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete(mwenye kofia) wametembelea maeneo ya mradi wa maji wa Chalinze, Kifuleta ,Pongwe Mnazi maji.Kazi ya kumaliza Kilio cha Maji Chalinze inakwenda kwa kasi kubwa kufuatia Serikali Kutenga Tshs.16 Bilioni kwa ajili ya ukamilishaji wa mradi wa maji ambao unatarajiwa kukabidhiwa mwezi wa nne mwaka 2020.