InfoChanyA+ MICHE MILLION 60 YA MITI IMEPANDWA KATIKA MASHAMBA TANZANIA.

WhatsApp Image 2018-10-15 at 17.00.13

Miche milioni 60 ya miti mbalimbali ilipandwa katika mashamba huku miche milioni 30 ikitolewa  wananchi na taasisi kwa ajili ya kupandwa

Kwa nini tunahitajika kupanda miti?
Tupande miti kwani maisha yetu yanategemea sana miti. Miti ni uhai.
Tunatakiwa kupanda miti na kuitunza ili ituletee faida.
Tupande miti ili tuokoe misitu yetu ya asili. Pia miti mingi inazuia mmomonyoko wa udongo na miti pia huzuia upepo mkali.
  • Fahamu aina mbalimbali za miti.
Miti ya matunda / chakula: miembe, miparachichi, mikorosho,
michungwa, mifenesi na michenza.
Miti ya mbao: mininga, mikongo, mivule, grevilea, mikangazi, mipaini na
mikaratuzi.
Miti ya kuni / nishati: mijohoro, grevilea.
Miti ya kurutubisha ardhi: grevilea, mikesya, milusina.
Miti ya dawa: milonge, miarobaini.
Miti ya chakula cha mifugo: milusina.
Miti ya kuhifadhi maji: mikuyu, mikangazi.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *