Meja Jenerali Martin Busungu, Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa nchini akikagua askari wa Kikosi cha JKT Mafinga mara baada ya kuwasili ili kukagua na kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazofanywa na kikosi hicho.
MKUU WA JKT AFANYA ZIARA YA KIKAZI KIKOSI CHA MAFINGA JKT
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Tanzania (JKT) Meja Jenerali Martin Busungu Ijumaa tarehe 05/10/2018 ametembelea kikosi cha JKT Mafinga na kukagua shughuli mbalimbali za uzalishaji mali zinazofanywa na kikosini hapo.
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Martin Busungu akisalimiana na maafisa wa Jeshi wa kikosi cha JKT Mafinga katika ziara yake ya kujitambulisha na kukagua shughuli mbalimbali za uzalishaji mali pamoja na mafunzo ya vikosi vya jeshi hilo.
Ziara hiyo ya Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa ni muendelezo wa ziara zake za kujitambulisha na kujionea shughuli za uzalishaji mali kwenye vikosi vya JKT nchini.
Pichani, Meja Jenerali Busungu akisalimiana na askari wa JKT katika kikoso cha Mafinga
Meja Jenerali Martin Busungu, Mkuu wa JKT akipata maelezo ya kitaalam kuhusu shughuli za ufugaji unaofanyika katika Kikosi cha JKT Mafinga – Mufindi mkoani Iringa.Meja Jenerali Busungu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kwenye Kikosi cha JKT Mafinga kwa ziara maalum ya kujitambulisha na kujionea shughuli za uzalishaji mali zinazofanywa na kikosi hicho cha jeshi analoliongoza.
Meja Jenerali Busungu akisikiliza maelezo kuhusu shughuli za kilimo alipoingia katika ghala la kuhifadhia chakula baada ya mavuno kwenya mashamba ya kikosi cha JKT Mafinga.
Mkuu wa jeshi la Kujenga Taifa nchini, Meja Jenerali Martin Busungu akipiga picha ya kumbukumbu na uongozi wa kikosi cha JKT MafingaMkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Busungu akiongea na askari wa kikosi cha JKT Mafinga.