Kongamano la wadau wa mazingira lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kufanyika tarehe 31 Mei 2024, katika Ukumbi wa JNICC, Dar es Salaam. Kongamano hili linakusudia kuleta pamoja wadau mbalimbali kujadili njia bora za kusimamia na kuhifadhi mazingira nchini Tanzania.
Mada kuu zitakazojadiliwa ni pamoja na:**
1. Kupunguza Athari za Mabadiliko ya Tabianchi:
– Mijadala itahusu jinsi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuchukua hatua za kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.
– Hii inajumuisha sera za nishati mbadala na mbinu za kilimo endelevu
2. Kuwajibika kwa Jamii:
– Kujadili njia za kuhakikisha jamii zinashirikishwa kikamilifu katika michakato ya usimamizi na uhifadhi wa mazingira.
– Elimu kuhusu umuhimu wa mazingira na kukuza ushirikiano kati ya serikali na jamii ni mambo muhimu yatakayozungumziwa
3. Uvumbuzi na Teknolojia:
– Kutambua na kukuza matumizi ya teknolojia na uvumbuzi katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira.
– Hii inajumuisha matumizi ya teknolojia ya kidijitali na vifaa vya kisasa vya kusafisha mazingira
Kongamano hili litatoa fursa kwa serikali, mashirika ya kiraia, sekta binafsi, na wananchi kushirikiana katika kutafuta suluhisho za kudumu za masuala ya mazingira nchini Tanzania.
Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+