
Rais Dkt. John Magufuli ameipandisha hadhi Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga kuwa Mansipaa ya Kahama, Rais Magufuli amesema hayo akiwa anazungumza na wananchi wa wilaya ya Kahama mkoani humo.
Rais Magufuli yupo kwenye Ziara ya kikazi mkoani humo ambapo ameweka jiwe la msingi katika kiwanda cha vinywaji baridi, nafaka na vifungashio cha KOM Food Products na pia ameweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Halmashauri ya mji wa Kahama.




Matokeo ChanyA+ Chombo kinachounga mkono matokeo yote chanyA+ TanzaniA+. #InfoChanyA+