NDEJEMBI AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKURABITA NA IDARA YA KUMBUKUMBU NA NYARAKA ZA TAIFA

Mratibu wa Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge nchini (MKURABITA) Dkt.Seraphia Mgembe akieleza utekelezaji wa mpango huo kwa Naibu Waziri ,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi wakati alipowatembelea katika ofisi zao viwanja vya nane nane nzuguni Dodoma ili kujitambulisha na kujua majukumu yao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mpango wa kurasimisha rasilimali na biashara za wanyonge nchini (MKURABITA) mara baada ya kuzungumza nao.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi akizungumza na watumishi wa Idara ya Kumbukumbu na Nyaraka za Taifa wakati alipowatembelea ili kujitambulisha na kujua majukumu yao.

Unaweza kuangalia pia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa na Askari wa Kikosi Kazi kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) walioshiriki Ujenzi wa Makao Makuu ya Ulinzi wa Taifa (MMUT), Kikombo Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *